23 Februari 2013 - 20:30

Ripoti na sanadi za hapa karibuni kutoka Tripoli zaeleza kua Muammar Ghaddafi alikuwa ameshaandaa jeshi kubwa Afrika na Mashariki ya kati kuvamia na kumpindua mfalme wa Saudia Arabia.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Ripoti za siri kutika Tripoli Libya zaonyesha kua Ghaddafi kabla ya kuuawa kwake alikuwa ameshaandaa jeshi kubwa Afrika na Mashariki ya kati kuvamia Saudia Arabia.

Kongozi huyo wa zamani wa Libya alikuwa aliajiri wapiganaji wa Somalia, Iraq na Yemen ambao walikuwa wanauhusiano Al-Qaida kwa kutaka kuangusha utawala wa Saudia.

Kulingana na ripoti ya gazeti moja la nchi hiyo liligawanya makundi ya Muammar Ghaddafi katika sehemu tatu, sehemu ya kundi la kwanza ni: Kaskazini mwa mashariki mwa Saudia. Kundi la Pili ni: Kaskazini mwa magharibi mwa Saudia. Kundi la Tatu ni: Kusini mwa Saudia. Na viongozi wa kila kundi alikuwa na uhusiano na serikali ya Saudia na kuandaa mashambulizi katika mikoa ya Riadh, Jiddah, Najran na Wajzan.

Ripoti hiyo ilieleza kua zaidi ya watu alfu 6 walofunzwa kutumia silaha katika kundi la kusini (katika yale makundi matatu) kila siku waendelea kuzidi na mwisho wake walifikia zaidi ya watu alfu 13 kundi hilo kulingana na ripoti ya gazeti.

Aidha katika makundi hayo kundi la kwanza liliomba milioni 6 dola $ hadi milioni 18 dola $, kundi la pili lilipewa milioni 7 dola $ na baadhi ya makabila ya Yemen kukabidhiwa milioni 7 dola $, na kundi la tatu kupewa kitita cha dola milioni 10 $ miongoni mwao hao ni kutoka Somalia na kila mmoja katika kila wapiganaji 1000 kupewa milioni 7/5 dola $.

Pia ripoti hii ilieleza kwamba kila kundi lilikuwa lishapewa bajeti na silaha kam R.P.G na grenade na silah ndogo ndogo ili kuandaa mapinduzi hayo, viongozi na wadasisi hao walikuwa wakiishi ndani ya Saudia Arabia ili kukusanya baadhi ya ripoti za awali, miongozi mwa maneno ya sanadi na ripoti za siri hizo imeelezwa kwamba: “SISI SI WAHARIBIFU AU KUTAKA KUMUAMSHA ADUI MJINGA ALOLALA LA HASHA ISIPOKUWA TWATAKA KULETA TIJA NZURI YA OPRESHENI HII.”